WATUMISHI HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA LINDI-SOKOINE WAPATIWA MAFUNZO KATIKA CHUMBA CHA UPASUAJI.

Posted on: February 9th, 2026

Watumishi wa hospitali ya rufaa mkoa wa Lindi-Sokoine wanapatiwa mafunzo katika chumba cha upasuaji na Bi.Salome Kassanga Afisa Muuguzi mbobezi katika chumba cha upasuaji.Mafunzo hayo yanaratibiwa na Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania kwa muda wa wiki mbili kuanzia tarehe 09/03/2026 hadi 22/03/2026.

Lengo la kutoa mafunzo hayo ni kuendeleza maarifa,ujuzi,umahiri na mitazamo chanya ya kitaaluma katika kutoa huduma salama za upasuaji pia kujenga uwezo kwa watoa huduma katika vyumba vya upasuaji.

Aidha,akizungumza na watumishi Bi.Salome amesema marajio baada ya mafunzo hayo ni pamoja na usalama kwa wagonjwa wanaofanyiwa upasuaji pia watoa huduma kuwa na umahiri wa kusimamia na kuendesha huduma katika vyumba vya upasuaji.