MGANGA MKUU WA MKOA DKT. VICTORINA AFANYA ZIARA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA SOKOINE - LINDI

Posted on: June 10th, 2026

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Lindi Dkt. Victorina Ludovick amefanya ziara yake ya kwanza katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa Sokoine ambapo ameweza kutembelea huduma zinazotolewa sambamba na maendeleo ya ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje.

Dkt. Victoria amefanya ziara hiyo leo 10/06/2026 akiambatana na timu ya usimamizi huduma za afya Mkoa.

Kupitia ziara hiyo Dkt. Victorina amewapongeza Menejimenti na Watumishi  kwa kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi licha ya ufinyu wa maeneo ya kutolea huduma.

Aidha amesema kuwa Uongozi wa Mkoa utaendelea kushirikiana na Menejimenti ya Hospitali, Wizara ya Afya kuhakikisha huduma zinaendelea kuimarika siku hadi siku kwa kuongeza miundombinu, huduma za kibingwa na kuifanya hospitali kuendelea kukidhi mahitaji ya wananchi wa mkoa wa Lindi kama Hospitali ya Rufaa ya Mkoa.