MADAKTARI BINGWA KUTOKA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA SOKOINE(LINDI) WAWEKA KAMBI KATIKA HOSPITALI YA WILAYA KILWA - KINYONGA.

Posted on: June 1st, 2026

Timu ya Madaktari bingwa na wataalamu mbalimbali kutoka katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Lindi - Sokoine wameweka kambi maalumu katika hospitali ya Wilaya ya Kilwa - Kinyonga na itadumu kwa muda wa siku nne kuanzia tarehe 01/06/2026 hadi 04/06/2026.

Lengo kuu la kambi hii ni kusogeza karibu huduma za kibingwa kwa wananchi wa halamashauri ya Kilwa itakayosaidia kuondoa adha ya kusafiri umbali mrefu kufuata huduma za kibingwa. 

Kambi hii inajumuisha huduma za kibingwa za magonjwa ya wanawake na uzazi, huduma za magonjwa ya watoto, huduma za upasuaji, huduma za kibingwa za magonjwa ya ndani, huduma za afya ya kinywa na meno pamoja na huduma za radiolojia na picha.


Akizungumza kwenye uzinduzi wa kambi hiyo Mganga Mfawidhi Dkt. Manda amesema kambi hii itasaidia kusogeza huduma kwa jamii na kufikia idadi kubwa ya wananchi wenye changamoto mbalimbali, kuwajengea uwezo watumishi wa hospitali hiyo.


Aidha, wananchi wamepokea vyema uwepo wa kambi hiyo kwa kujitokeza kwa wingi kwaajili ya kupata huduma