SPECIALTIES

IDARA YA UPUSUAJI MCHANGANYIKO

Jina la Mkuu wa Idara: Dkt. Joseph Mwiru

Namba ya simu:

Barua pepe:

Hii ni idara ni moja kati ya idara 12 za Hospitali ya Sokoine, hii idara ina mamlaka ya kuwahudumia wagonjwa wote wenye uhitaji wa upasuaji wagonjwa wa nje na wanaolazwa. Hii idara imegawanyika kulingana na vitengo mbalimbali:-

  • Kitengo cha Masikio na, Pua na koo
  • Kitengo cha Macho na
  • Kitengo cha Kinywa na Meno

Idara hii ina majukumu ya kutoa huduma bora ya hali ya juu kwa wateja wake


MACHO NA UONI HAFIFU

Wagonjwa wote wenye manamatizo ya kutoona mbali au karibu hutibiwa mataizo hayo kwa kutumia miwani au vifaa vingine kama vile darubini lenzi ya kukuza muonekano wa vitu.Aina zote za miwani / vifaa hupatikana kutegemana na chaguo la wagonjwa,kitengo hichi hufanya kazi kila siku kuanzia saa 1:30 asubuhi  hadi 9:30 mchana.

SHUGHULI ZA KITENGO

  • Upasuaji mdogo wa kuweka kipokezi ( phaco) na kupandikiza kipakio( IOL)
  • Upasuaji
  • Upasuaji wa ugonjwa unaoathiri neve za macho(Glaucoma surgery)
  • Uchunguzi wa magonjwa yanayoathiri Retina.
  • Upasuaji wa mtoto wa jicho.
  •  Magonjwa ya konea, hali na maumivu.
  • Kukaa kwa siku/upasuaji wa wagonjwa wa ndani( inpatient surgery)
  • FFA ( fundus fluorescein angiography)
  • Glaukoma
  • Upasuaji mdogo
  • Uchunguzi wa awali ( pre- assessment)
  • Uchunguzi wa retina
  • Kusafisha tezi za macho
  • Uoni
  • Upasuaji wa vireo- retina

WATUMISHI

Kitengo kinawatumishi wanne (4) walioajiliwa, ambao ni kama hujumuisha:-

  • Daktari wa upasua wa macho( Ophamology surgeon)     1
  • Nesi wa macho (Ophamology nurse)                                1
  • Fundi sanifu wa miwani                                                     1
  • Muhudumu                                                                        1

SHUGHURI ZA IDARA KWA UJUMLA

Kwa ufupi, shughuri zinazofanywa na Idara ni:-

  • Kutoa huduma boara, ya ufanisi naya kiwango cha juu kwa wagonjwa.
  • Kutoa huduma za macho kwa usalama na kiwango cha juu.
  • Kufanya mafunzo kazini na kupanga ratiba mbalimbali hasa za usalama katika utoaji huduma na matibabu ya macho endelevu.
  • Kufanya uchunguzi wa  kisayansi ( operational and scientific research)
  • Kuhudumia wagonjwa wote wa dharula wanoletwa hospitalini.
  • Kutoa ushauri kwa wagonjwa wanaokuja wenyewe kwa ajili ya matibabu au wagonjwa wa rufaa na wagonjwa wengine wanaokuja kwa ajili ya muendelezo wa matibabu ( follow up)
  • Kufundishi wanafunzi wanosomea udaktari, unesi na wanafunzi wageni wanaotembelea.
  • Kutoa huduma sehemu za mbali ziliko ndani ya mkoa ( outreach services)
  • Kufundisha na kutoa ushauri katika vituo vya kutolea huduma ya za afya ili kuimarisha ya za macho katika mkoa.

Kliniki katika Idara

Kliniki ya macho hutoa huduma kuanzia jumatatu hadi ijumaa siku za wiki.


KITENGO CHA KINYWA NA MENO

Kitengo cha meno kimegawanyika katika sehemu tatu;

  • Sehemu Upasuaji
  • Sehemu ya kurudishia jino kwenye hari yake ya mwanzo ( Restorative)
  • Sehemu ya matibabu ya watoto na urekebishaji wa meno

Kliniki ya wagonjwa wa nje

Hii ni sehemu ya kuanzia ambapo wagojwa huelekezwa kwenye kwenye kliniki husiku,wagonjwa wanaohdhuria kwenye kliniki hii ni wagonjwa wapya ambao wamekuja wenyewe au wa rufaa na wale wagonjwa wanaoruhusiwa kutoka wodini.

Hawa ni wagonjwa wanaokuja na meno yaliyotoboka sana, meno yameota vibaya,wenye matatizo ya fizi, ambao hawana meno, wenye matatizo baada kupata  matibabu, jipu la jino, maumivu na kuumia , maumivu sehemu ya ya uso na uvimbe.

Wagonjwa wenye matatizo zaidi, hujadiliwa na Daktari kwa ajili ya kufanya upasuaji, upasuaji wa kurudishia sehemu iliyoharibika, na kurufaa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu zaidi.

Wagonjwa huchunguzwa ili kutafuta chanzo cha tatizo, huchunguzi wa kinywa na mwili kwa ujumla na kufanyiwa vipimo vinavyoendana na tatizo mfano x- ray,kipimo kwa ajili ya meno ya bandia hufanyika. Baadae matibabu hufanyika na mgonjwa huambiwa sababu, dalili na kujikinga juu ya tatizo lake ikilenga hasa jinsi ya kusafisha kinywa na matibabu mengine ili kuzuia kutokea tena kwa magonjwa ya kinywa na meno.Kwa watoto wenye uvimbe hupelekwa kwenye kitengo upasuaji kwa uchunguzi na matibabu.

KITENGO CHA KUZIBA MENO

Wagonjwa hawa ni wale ambao meno yao yametoboka yamefikia neva, matatizo ya fizi,halafu mbaya kinywani,kukosa meno,meno yaliyopoteza rangi,kuumia. Wagonjwa huchunguzwa ili kutafuta chanzo cha tatizo, huchunguzi wa kinywa na mwili kwa ujumla na kufanyiwa vipimo vinavyoendana na tatizo mfano x- ray,kipimo kwa ajili ya meno ya bandia hufanyika. Baadae matibabu hufanyika na mgonjwa huambiwa sababu, dalili na kujikinga juu ya tatizo lake ikilenga hasa jinsi ya kusafisha kinywa na matibabu mengine ili kuzuia kutokea tena kwa magonjwa ya kinywa na meno.Kwa watoto wenye uvimbe hupelekwa kwenye kitengo upasuaji kwa uchunguzi na matibabu

Watumishi

Idara in watumishi sita miongoni mwao wawili ni Madaktari wa upasuaji na wanne ni wafanyakazi wengine

SHUGHURI ZA IDARA KWA UJUMLA

Kwa ufupi, shughuri zinazofanywa na Idara ni:-

  • Kutoa huduma boara, ya ufanisi naya kiwango cha juu kwa wagonjwa.
  • Kutoa huduma za kinywa na meno kwa usalama na kiwango cha juu.
  • Kufanya mafunzo kazini na kupanga ratiba mbalimbali hasa za usalama katika utoaji huduma na matibabu ya macho endelevu.
  • Kufanya uchunguzi wa  kisayansi ( operational and scientific research)
  • Kuhudumia wagonjwa wote wa dharula wanoletwa hospitalini.
  • Kutoa ushauri kwa wagonjwa wanaokuja wenyewe kwa ajili ya matibabu au wagonjwa wa rufaa na wagonjwa wengine wanaokuja kwa ajili ya muendelezo wa matibabu ( follow up)
  • Kufundishi wanafunzi wanosomea udaktari, unesi na wanafunzi wageni wanaotembelea.
  • Kutoa huduma sehemu za mbali ziliko ndani ya mkoa ( outreach services)
  • Kufundisha na kutoa ushauri katika vituo vya kutolea huduma ya za afya ili kuimarisha ya za macho katika mkoa.

Kliniki katika Idara

Kliniki ya macho hutoa huduma kuanzia jumatatu hadi ijumaa siku za wiki.