laboratory

IDARA YA MAABARA

Mkuu wa idara. Godfrey Chotta

Kitengo cha maabara kimegawanyika katika sehemu tano ambazo ni

  • Microbiology na immunology
  • Hematology na blood transfusion
  • Parasitology na Entomology
  • Clinical Chemistry na Molecular Biology
  • Chumba ya kuhifadhia maiti

Hivi vitengo vyote vipo ndani ya jengo moja la maabara isipokuwa chumba cha kuhifadhia maiti ina jengo linalo jitegemea. Katika kitengo hiki cha maabara kinafanya kazi kubwa na muhimu kuhakikisha kinatoa majibu sahihi na kwa mtu sahihi. Sehemu zote zimeungnishwa na mfumo wa serikali GoT-HoMIS ambao unawezesha madakrari kuwasiliana na maabara bila kutumia makaratasi, na majibu yanatumwa kwa njia ya mtandao huo, hivyo kufanya majibu ya mgonjwa kuwa siri zaidi.

SEHEMU YA KWANZA MICROBIOLOGY NA IMMUNOLOGY

Katika kitengo hiki hufanyika uchunguzi kwa njia kuotesha vimelea na kasha kuangalia hivyo vimelea vinaweza kufa kwa dawa gani. Hapa pia uchunguzi wa magonjwa mbalimbali kupitia maji maji ya damu unafanyika kama vile homa ya matumbo, kaswende, vimelea vinavyo sababisha vidonda vya tumbo, tezi dume na kadhalika.

SEHEMU YA PILI HAEMATOLOGY NA BLOOD TRANSFUTION

Hapa kuna vipomo vingi ikiwemo kuangalia picha ya damu (FBP) ili kugundua sababu ya upungufu wa damu, kipimo cha selimuntu (sickling test) na maonjwa mengine ya damu ikiwemo kansa ya damu. Pia sehemu hii inashughulika na kuongeza damu kwa wagonjwa wenye uhitaji. Pia wanaotakiwa kufanyiwa upasuaji. Sehemu hii ina mashine mbili , moja kubwa inayotumika mda wote na nyingine ndogo ambayo inatumika wakati ile kubwa ipo kwenye matengenezo.

SEHEMU YA TATU PARASITOLOGY NA ENTOMOLOGY

Sehemu hii inahusika na uchunguzi wa magonjwa ya minyoo na vimelea vya maralia na mengine kwenye damu,  mkojo na haja kubwa.

SEHEMU YA NNE CLINICAL CHEMISTRY

Katika sehemu hii inatumika mashine mbalimbali  kwa ajili ya kufuatilia utendaji kazi wa viungo mbalimbali vya mwili mfano:- INI, FIGO, MOYO, UBONGO Via vya Uzazi na vingine vingi.

SEHEMU YA TANO CHUMBA CHA KUHIFADHIA MAITI

Hii ni sehemu ambayo inashughulika na uhifadhi wa maiti, kuweka dawa ili maiti isiharibike, kusafisha na kupamba. Kuna majokofu mawili yenye uwezo wa kuhifadhi maiti sita kwa kila moja